0 votes
170 views
in General by
closed
170 views
closed

12 Answers

0 votes
by (149k points)

W
335.       Wake wa mjomba kimo kimoja. Vipande vya kweme

336.       Wako karibu lakini hawasalimiani. Nyumba ama kuta zinazoelekeana
337.       Wanakuja mmoja mmoja na kujiunga kuwa kitu kimoja. Matone ya mvua
338.       Wanameza watu jua linapokuchwa. Nyumba
339.       Wanamwua nyoka. Watu wanaotwanga
340.       Wanangu wawili hugombana mchana, usiku hupatana. Mlango
341.       Wanao wakati wao wa kuringa, nao ni weupe kama barafu. Nyota
342.       Wanapanda mlima kwa makoti mazuri meusi na meupe. Vipepeo
343.       Wanastarehe darini. Panya
344.       Wanatembea lakini hawatembelewi. Macho
345.       Watoto wa mtu mmoja hulala chini kila mwaka. Maboga
346.       Watoto wangu wana vilemba, asio kilemba si mwanangu. Fuu
347.       Watoto wangu wote nimewavika kofia nyekundu. Jogoo
348.       Watoto wangu wote wamebeba vifurushi. Vitovu
349.       Watu ishirini walipanda juu ya mti, wawili wakaona chungwa, watano wakalichuma, kumi wakalimenya, wote wakaridhirika mtu mmoja alile. Je, ni watu gani hao? Waliopanda ni vidole vya miguu na mikono, walioona ni macho mawili, waliochuma ni vidole vitano vya mikono, waliomenya ni vidole vya mikono yote miwili, na aliyelila ni mdomo
350.       Watu waliokaa na kuvaa kofia nyekundu. Kuku, katani au mahindi
351.       Watu wamehama askari wekundu wakazidi nyikani. Viroboto
352.       Watu wawili hupendana sana; kati ya mchana hufuatana ingawa mmoja ni dhaifu. Usiku mdhaifu
haonekani tena. Kivuli
353.       Watu wote ketini tumfinye mchawi. Kula ugali
354.       Wewe kipofu unaenda wapi huko juu? Mkweme

0 votes
by (149k points)

Y
355.       Yaenda mbali lakini haiondoki ilipo. Njia

Z
356.       Zilitazamana na mpaka sasa hazijakutana. Kingo za mto
357.       Ziwa dogo linarusha mchanga. Chungu jikoni
358.       Ziwa kubwa, lakini naogelea ukingoni tu. Moto

Related questions

0 votes
1 answer 12 views
asked 6 days ago in General by kennedy 12 views
0 votes
1 answer 18 views
0 votes
1 answer 38 views
0 votes
1 answer 44 views
0 votes
1 answer 50 views
0 votes
1 answer 35 views
asked Aug 28 in General by Zilper 35 views
0 votes
0 answers 24 views
0 votes
1 answer 76 views
0 votes
0 answers 33 views
0 votes
1 answer 80 views
0 votes
1 answer 42 views
0 votes
1 answer 38 views
asked Aug 20 in General by kevin (437k points) 38 views
Welcome to Nestict Research Q&A, where you can ask questions and receive answers from other members of the community.

Before you ask, search the website to make sure your question has not been answered. If you are ready to ask, provide a title about your question and a detailed description of your problem.

...